1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON : Marekani kutaka Moussaoui ahukumiwe kifo

23 Aprili 2005

Mwanasheria Mkuu wa serikali Alberto Gonzales amesema serikali ya Marekani itataka Zakaria Moussaoui mwanachama wa kundi la Al Qaeda ahukumiwe kifo kufuatia kukiri kwake hapo jana kula njama kuhusiana na mashambulizi ya kigaidi ya Septemba 11 dhidi ya Marekani.

Gonzales amesema ukweli kwamba Moussaoui alishiriki katika njama hiyo ya kigaidi sio tena jambo la kutiliwa mashaka na kwamba yeye na wala njama wenzake walihusika na vifo vya maelfu ya Wamarekani wasiokuwa na hatia hapo Septema 11.

Moussaoui Mfaransa mwenye asili ya Morroco mwenye umri wa miaka 36 ambaye ni mtu pekee anayeshtakiwa kwa mashambulizi ya Septemba 11 nchini Marekani amekiri kuwa na hatia kwa mashtaka yote sita ikiwa ni pamoja na kula njama za kufanya ugaidi,kuteketeza ndege, kutumia silaha za maangamizi makubwa na mauaji.

Wakati akikiri kuwa na hatia Moussaoui ameahidi kupinga kwa njia zote zile hukumu ya kifo.

Habari hizo zinakuja wakati kesi nyengine ikiendelea nchini Uhispania dhidi ya watuhumiwa 24 wanachama wa tawi la Al Qaeda nchini humo ambapo wanne kati yao wanashtakiwa kwa kusaidia, kupanga na kugharimia mashambulizi ya kigaidi ya Septemba 11 mwaka 2001 nchini Marekani.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW