1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON: Marekani na Ufaransa zinafanya hima ya kutaka kuboresha ...

16 Januari 2004
upya uhusiano wao uliodorora. Kwa mara ya kwanza tangu vita vya Irak, waziri wa ulinzi wa Marekani Donald Rumsfeld alikutana kwa saa moja na mwenzake wa Ufaransa Bibi Michele Alliot-Marie. Msemaji wake alitamka, mkutano huo mjini Washington umefanyika kwa moyo mwema wa kutaka ushirikiano, lakini hajaelezea zaidi. Ufaransa ilikuwa miongoni mwa nchi zilizopinga vita vya Irak, kama Urussi na Ujerumani.