1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Washington. Marekani na umoja wa Ulaya washindwa kufikia muafaka.

1 Oktoba 2006

Umoja wa Ulaya na Marekani zimeshindwa kupata muafaka katika makubaliano ya mwisho juu ya kupashana taarifa za takwimu za wasafiri wa ndege ilipofika siku ya mwisho jana Jumamosi.

Waziri wa usalama wa nchi wa Marekani , Michael Chertoff amewaambia waandishi wa habari kuwa ametuma muswada wa makubaliano kwa wawakilishi wa umoja wa Ulaya , lakini msemaji wa tume ya Ulaya mjini Brussels amesema kuwa majadiliano yanayofanyika mjini Washington yameshindwa kutoa makubaliano.

Pande zote mbili zimesema kuwa ziko tayari kuendelea na mazungumzo.

Makubaliano hayo yanatakiwa na Marekani ili kuzuwia mashambulizi ya kigaidi. Mahakama ya Ulaya mwezi wa May ilitoa hukumu kuwa makubaliano yaliyopo , ambayo yanayataka makampuni ya usafiri wa ndege ya ulaya kutoa aina 34 ya takwimu kwa ajili ya wasafiri wanaoelekea nchini Marekani kwa maafisa wa Marekani, ni kinyume na sheria kwasababu haijakubalika kwa misingi ya mfumo wa sasa wa sheria za umoja wa Ulaya.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW