WASHINGTON : Marekani yaionya Sudan
28 Septemba 2006Matangazo
Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Condoleezza Rice amemuonya Rais Omar al Bashir wa Sudan kwamba serikali yake inakabiliana na matokeo ya madhara asiyoyataja iwapo wanajeshi wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa hawatoruhusiwa kuwekwa kwenye jimbo lilioathirika na vita la Dafur.
Akizungumza katika mkutano wa Jumuiya ya Afrika mjini Washington Rice ameongeza kusema iwapo Rais Bashir ataamuwa kushirikiana na Umoja wa Mataifa Sudan itaiona Marekani ni mshirika makini.Rice pia ameishutumu serikali ya Sudan kwa kuendesha vita dhidi ya raia zake,kuupinga Umoja wa Afrika na kuitishia jumuiya ya kimataifa.
Hata hivyo mwanadiplomasia huyo mkuu wa Marekani ameweka wazi kwamba Marekani haina nia ya kuishambulia serikali ya Sudan.