WASHINGTON: Marekani yaishuku Syria kwa mauaji Lebanon.
14 Juni 2007Matangazo
Marekani imetoa matamshi yanayoashiria inashuku Syria imehusika na shambulio la bomu la jana mjini Beirut lililowaua watu kumi akiwemo mbunge wa Lebanon ambaye anaipinga Syria.
Rais George W Bush wa Marekani amesema mauaji hayo yanafanana sana na mauaji na pia majaribio ya mauaji ambayo yameendelea nchini Lebanon tangu mwaka 2004.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moo, amesema mauaji hayo ni uhalifu wa hali ya juu uliolengwa kuisambaratisha nchi hiyo.