1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON: Marekani yaiwekea Zimbabwe vikwazo zaidi

4 Agosti 2005

Marekani imetangaza vikwazo zaidi dhidi ya serikali ya Zimbabwe katika hatua inayodhamiriwa kuwatenga viongozi wanaotatiza demokrasi katika mataifa ya Afrika.

Wizara ya fedha nchini Marekani imezitenga ili kuzifanyia uchunguzi kampuni 26 za Zimbabwe ambazo zinaendeshwa na watu muhimu katika utawala wa serikali ya Mugabe.

Robert Werner Mkurugenzi wa ofisi inayosimamia raslimali za kigeni nchini Marekani OFAC amesema hatua hiyo itaukata usaidizi ambao huenda ukatumiwa na Mugabe kuilemaza zaidi nchi ya Zimbabwe.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW