1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON: Marekani yataka Syria ichukuliwe hatua kwa kifo cha Hariri

22 Oktoba 2005

Waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani, Condoleezza Rice, anataka Syria ichukuliwe hatua baada ya maofisa wake wa ngazi ya juu kutajwa katika ripoti ya umoja wa mataifa kuhusu uchunguzi wa kifo cha waziri mkuu wa zamani wa Lebanon, Rafik Hariri.

Ripoti hiyo iliyotayarishwa na mchunguzi kutoka Ujerumani, Detlev Mehlis, itajadiliwa na baraza la usalama la umoja wa mataifa mjini New York, Marekani, Jumanne wiki ijayo.

Kwa upande wake Syria inapinga kuhusika katika shambulio la bomu lililomuua Hariri na watu wengine 20 mwezi Februari mwaka huu, ikisema ripoti hiyo ina msukumo wa kisiasa. Ripoti hiyo pia imetaja ushahidi ulio wazi kwamba Syria na Lebanon zilihusika na kuilaumu serikali ya Damascus kwa kuzuia na kupotosha uchunguzi wa kifo hicho.

Rais wa zamani wa Lebanon, Amin Gemayel, anataka watuhumiwa waliohusika na kifo cha Hariri wafikishwe mbele ya mahakama ya kimataifa. Amesema, akiwa nchini Ufaransa, kwamba ni muhimu kuwajua waliosababisha vifo hivyo ili kuikaribisha enzi mpya ya uhuru na demokrasia nchini Lebanon.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW