Washington. Mlinzi wa Osama bin laden sasa kushitakiwa katika mahakama ya kijeshi.
16 Julai 2005Matangazo
Mahakama moja ya rufaa nchini Marekani imeamua kuwa mfungwa mmoja katika jela ya kuwaweka mahabusu ya Guantanamo Bay anayetuhumiwa kuwa ni mlinzi wa Osama bin Laden , kesi yake inaweza kufanyika katika mahakama ya kijeshi, na kufuta uamuzi wa hapo awali katika mahakama ya chini kuwa kesi hiyo kusikilizwa katika mahakama ya kijeshi ni kinyume na sheria na itakwenda kinyume na haki zake.
Ikiwa ni ushindi kwa utawala wa rais Bush , jopo la majaji watatu limesema kuwa mahakama hiyo ya kijeshi katika kituo cha kijeshi cha Marekani cha Guantanamo Bay , Cuba ni sehemu sahihi kwa Salim Ahmed Hamdan kushitakiwa.
Hamdan ameshitakiwa kwa kula njama za kushambulia raia, kuuwa, kuharibu mali na ugaidi.