1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON: Mwanasheria Mkuu anataka adhabu ya kifo kwa Moussaoui

23 Aprili 2005

Zacarias Moussaoui,mtu pekee kushtakiwa nchini Marekani kuhusu mashambulio ya Septemba 11 mwaka 2001,amekiri kuwa na hatia ya kuhusika na njama ya wanachama wa kundi la Al-Qaeda.Moussaoui,raia wa Ufaransa mwenye asili ya Kimoroko,anakabiliwa na mashtaka 6 mbali mbali.Mashtaka 4 yana adhabu ya kifo.Mwanasheria Mkuu wa Marekani amesema anataka kuona kuwa Moussaoui anapewa adhabu ya kifo.Muda mfupi kabla ya mashambulio ya Septemba 11,Moussaoui alikamatwa kwa makosa yanayohusika na viza.Alisababisha wasi wasi baada ya kuchukua mafunzo ya kurusha ndege kwenye shule ya kutoa mafunzo hayo nchini Marekani,ambayo ilitumiwa pia na baadhi ya marubani waliojitolea kufa na kuishambulia miji ya New York na Washington.Moussaoui amekanusha kuhusika na njama ya Septemba 11,lakini amekiri kuwa alishiriki katika njama nyingine ya kuishambulia Ikulu mjini Washington.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW