1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON Ndege ya Marekani yaanguka kusini mwa Asia

23 Juni 2005

Rubani wa ndege ya jeshi la angani la Marekani amefariki dunia baada ya ndege iliyotumiwa kufanya upelelezi kuanguka kusini magharibi mwa Asia.

Duru za jeshi la Marekani zinasema, ndege hiyo ilianguka wakati rubani huyo alipokuwa akirudi kambini baada ya kumaliza kazi yake katika juhudi zao za kuwasaidia wanajeshi wa Marekani walio nchini Afghanistan. Msemaji wa jeshi ametangaza kwamba mahala ilipoanguka ndege hiyo hapatatangazwa kwa sababu ya usalama wa taifa hilo.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW