WASHINGTON: Obama kulitembelea bara la Afrika
27 Julai 2006Matangazo
Seneta wa Marekani katika chama cha Democrats, Barack Obama, kutoka jimbo la Illinois na ambaye ni mtoto wa mkenya, amesema atayatembelea mataifa matano ya Afrika mwezi ujao kusaidia kuboresha maendeleo ya kisiasa na kiuchumi barani Afrika.
Obama, mwafrika mweusi pekee katika baraza la senate, amewahi kuwatembelea jamaa zake nchini Kenya, lakini ziara hii itakuwa ya kwanza rasmi.
Obama ataizitembelea Kenya, Afrika Kusini, Kongo, Sudan na Djibouti kati ya Agosti 18 na tarehe 2 Septemba.