WASHINGTON: Olmert amewasili Marekani kwa mazungumzo na Bush
12 Novemba 2006Matangazo
Waziri mkuu wa Israel,Ehud Olmert amewasili Washington nchini Marekani kwa mkutano wake wa pili pamoja na rais George W.Bush.Mkutano huo umepangwa kufanywa siku ya Jumatatu.Kufuatia matokeo ya hivi karibuni ya uchaguzi wa bunge nchini Marekani,Olmert amesema anataka kujiarifu juu ya siasa ya Washington kuhusu mgogoro wa Waisraeli na Wapalestina.Suala la Iran pia linatarajiwa kuchukua nafasi muhimu katika mazungumzo ya viongozi hao wawili.