1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON: Osama bin Laden ajitokeza kwenye kanda ya video

15 Julai 2007

Kiongozi wa Al-Qaeda,Osama bin Laden amejitokeza kwenye kanda ya video isiyo na tarehe,baada ya kutosikika wala kuonekana mwaka mzima.Bin Laden anaeonekana kwa dakika moja katika kanda hiyo yenye urefu wa dakika 40 katika tovuti ya wanamgambo,anawasifu wale wanaokufa mashahidi.Kwa mujibu wa kundi la ujasusi la SITE lenye makao yake mjini Washington,kanda hiyo ya video ni ya zamani lakini hakuna tarehe iliyokisiwa.Kwenye kanda hiyo ya video kulikuwepo pia risala kutoka viongozi wengine wa Al-Qaeda nchini Afghanistan. Juma lililopita Seneti ya Marekani iliongeza maradufu,pesa zitakazotolewa kwa habari zitakazomkamatisha Osama bin Laden.Sasa idadi hiyo ni Dola milioni 50.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW