WASHINGTON: Palestina yatakiwa kuikubali Israel ili ipewe msaada
22 Machi 2007Matangazo
Kundi la madalali wa amani huko mashariki ya kati, limeitaka serikali ya kitaifa ya Palestina kutangaza kuachana na vurugu na pia kukubali haki ya kuwepo kwa taifa la Israel.
Katika taarifa yao iliyotolewa kwa niaba ya Marekani, limesema kuwa vikwazo vya moja kwa moja vya misaada dhidi ya mamlaka ya Palestina vitaendelea kuwepo mpaka hapo, serikali hiyo itakapotimiza masharti hayo.
Hii ni taarifa ya kwanza ya kundi hilo toka kuundwa kwa serikali ya kitaifa, ambayo inaundwa na makundi ya Fatah na Hamas.
Kundi hilo la madalali wa amani huko mashariki ya kati linaundwa na Umoja wa Mataifa, Umoja wa Ulaya, Marekani na Urusi.