1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON: Rais Bush akataa kutangaza tarehe ya kuwaondoa wanajeshi kutoka Irak

20 Julai 2005

Rais George W Bush wa Marekani na waziri mkuu wa Australia, John Haward, wamekataa mwito wa kutangaza tarehe ya kuwaondoa wanajeshi wao kutoka Irak. Akizungumza katika ikulu ya white house baada ya mazungumzo yake na Haward, rais Bush amesema wanajeshi wa Marekani na jeshi la muungano hawataondoka Irak mpaka wakamilishe kazi yao.

Viongozi hao pia wameupongeza mkataba wa biashara huru ulioanza kufanya kazi Januari mosi mwaka huu. Bush alijadili kuhusu mazungumzo ya mataifa sita yanayolenga kukomesha mpango wa nuklia wa Korea Kazkazini.

Rais Bush pia amemteua jaji John Roberts kuwa jaji katika mahakama kuu. Roberts mwenye umri wa miaka 50, ataichukua nafasi yake Sandra Day O´Connor, iwapo ataidhinishwa na bunge.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW