1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON: Rais Bush kuzuru barani Asia juma lijalo

9 Novemba 2005

Rais George W Bush wa Marekani amesema atataka ushirikiano wa karibu na Asia katika vita dhidi ya ugaidi na homa ya ndege na kuimarisha demokrasia wakati wa ziara yake barani Asia wiki ijayo.

Rais Bush anatarajiwa kuzitembelea Japan, China, Korea Kusini na Mongolia na kuhudhuria mkutano wa kilele wa mataifa 21 wanachama wa ushirikiano wa kiuchumi wa mataifa ya Asia na Pacific, APEC. Mkutano huo utakaotuwama juu ya juhudi za kuboresha biashara ya kimataifa, umepangwa kufanyika mji mkuu wa Korea Kusini, Busan.

Bush atalijadili swala nyeti la haki za binadamu na rais wa China, Hu Jintao na kumtaka awache kuishusha thamani ya sarafu ya nchi hiyo, hatua ambayo Marekani inasema inazifanya bidhaa za China kununuliwa kwa wingi katika masoko ya kimataifa.

Wakati huo huo, rais Bush amethibitisha kwamba mkataba mpya wa kulifunganisha jeshi la Marekani nchini Japan unapingwa na wengi huko Okinawa ambako kuna wanajeshi wengi wa Marekani. Hata hivyo rais Bush amesema Marekani na Japan zinatafuta suluhisho la mzozo huo.