1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON: Ripoti ya Marekani kuhusu kifo cha ajenti wa Kitaliana

1 Mei 2005

Jeshi la Marekani limetoa ripoti isiyokubaliwa, kuwa hakuna hatua itakayochukuliwa kuwaadhibu wanajeshi waliompiga risasi na kumuuwa ajenti wa Kitaliana mjini Baghdad.Uamuzi huo bila shaka utazidisha mkwaruzano kati ya Washington na Rome ambayo siku ya Jumatatu itatoa ripoti yake yenyewe baada ya kushindwa kukubaliana na mahitimisho ya uchunguzi wa pamoja.Kifo cha ajenti Nicola Calipari kilitokea tarehe 4 mwezi wa Machi,alipokuwa akimsindikiza mwandishi wa habari wa Kitaliana alieachiliwa huru na wanamgambo hapo punde tu na gari yao kupigwa risasi na vikosi vya Marekani karibu na uwanja wa ndege wa Baghdad.Marekani imesema wanajeshi wake walichukua hatua kuambatana na sheria za kazi yao na kifo cha Calipari ni „ajali inayosikitisha.“

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW