Washington Robert Chiula, Afrika Kusini
23 Mei 2013Matangazo
"Ninaushangiria Umoja wa Afrika: Umepambana dhidi ya ukoloni na hapa nchini Afrika ya Kusini umeutokomeza utawala wa ubaguzi wa rangi na mtengano. Katika enzi za ubaguzi wa rangi na mtengano sikuwa na ruhusa mie ya kuchagua kazi nnayotaka kufanya, baadhi ya njia nilikuwa siruhusiwi kupita - sikuwa na ruhusa ya kumiliki nyumba wala gari. Hivi sasa vyote hivyo nnaweza kuwa navyo. Watoto wangu wanakwenda shule waitakayo. Nina kampuni yangu mwenyewe na ninaweza kuwaajiri hata wafanyakazi wenye asili ya Kizungu."