WASHINGTON: Serikali ya Iran itashinikizwa zaidi
21 Septemba 2007Marekani na Ufaransa zinataka kuishinikiza zaidi serikali ya Iran kuhusu miradi yake ya nyuklia. Hata hivyo,Rais George W.Bush wa Marekani amesema,bado ana matumaini ya kuisadikisha Iran, kuachilia mbali mipango yake ya nyuklia kwa njia za kidiplomasia.
Rais Bush amesema,wataendelea kuishinikiza Iran.Juu ya hivyo,lengo ni kupata suluhisho la amani.
Hata Waziri wa Masuala ya Nje wa Ufaransa,Bernard Kouchner ameimarisha msiamamo wake kuhusu mgogoro wa nyuklia.Alipozungumza mjini Washington, Kouchner alisema,Iran iliyo na silaha za nyuklia, ni wazo lisilokubalika.Leo Ijumaa,wajumbe wa nchi tano zenye kura turufu katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa pamoja na Ujerumani, wanakutana mjini Washington,kushauriana juu ya uwezekano wa kuweka vikwazo zaidi dhidi ya Iran.