WASHINGTON: US kubakisha vikwazo dhidi ya Libya
6 Januari 2004Matangazo
Marekani imesema kuwa itaendelea kuiwekea Libya vikwazo hadi pale itakapothibitika kuwa serikali ya Tripoli imetimiza ahadi yake ya kuzima harakati zake za kuunda silaha za sumu na nuklia. Rais George W. BUSH amesema hata hivyo kuwa Marekani inaamini kuwa Libya inakusudia kutekeleza kikamilifu ahadi hizo huku akiiomba kuzingatia wasiwasi huo wa serikali ya Washington. Vikwazo hivyo ni pamoja na kuizuwia Libya kutumia akiba yake ya mabilioni ya Dola yaliyowekwa katika mabenki ya Marekani. Mwezi uliopita, Libya ilitangaza nia ya kuachana na mradi wake wa silaha zilizopigwa marufuku kimataifa na kuamua kuwaalika wachunguzi wa silaha wa kimataifa kukagua vinu vyake vya kinuklia.
