1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON: Vikosi vya kimataifa vilinde usalama

29 Julai 2006

Marekani na Uingereza zinataka kuvimaliza vita vya kusini mwa Lebanon upesi iwezekanavyo kwa kupeleka vikosi vya kimataifa kulinda amani katika eneo hilo.Rais George W.Bush wa Marekani, baada ya kukutana na waziri mkuu wa Uingereza,Tony Blair mjini Washington,alisema, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa litakutana Jumatatu ijayo kujadili pendekezo la kutuma kikosi cha Umoja wa Mataifa kulinda usalama.Vile vile aliarifu kuwa waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani,Condoleezza Rice atarejea Mashariki ya Kati siku ya Jumamosi kujadiliana na viongozi wa Israel na Lebanon.Hakuna hata mmoja kati ya viongozi hao wawili alietoa mwito wa kusitisha moja kwa moja mapigano,kati ya Israel na Hezbollah.Bush na Blair wanasisitiza haja ya kuwepo suluhisho la muda mrefu na kwa wanamgambo wa Hezbollah kutokuwa na mahala pa kujificha kusini mwa Lebanon.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW