WASHINGTON: Wageni wanaozuru Marekani kupigwa picha
5 Januari 2004Matangazo
Kuanzia leo siku ya Jumatatu wageni wanaoitembelea Marekani watapigwa picha na kuchukuliwa alama zao za vidole kama sehemu ya mfumo mpya wa kuimarisha usalama nchini humo. Mpango huo unaoitwa Ziara-Marekani utawaathiri abiria wanaowasili katika viwanja vyote vya ndege 115 ambavyo huhudumia ndege za kimataifa pamoja na bandari kuu 14.Zaidi ya watu milioni 28 watakumbwa na mpango huo kwa mwaka. Hata hivyo hatua hizo za kuimarisha usalama hazitowaathiri raia wa Umoja wa Ulaya, raia wa Japani na wengine ambao kwa kawaida huruhusiwa kuitembelea Marekani bila ya kuhitaji visa.