Washington. Wamarekani weusi waandamana.
16 Oktoba 2005Matangazo
Mamia kwa maelfu ya Wamarekani weusi wameandamana dhidi ya hali ya kutokuwa na usawa nchini humo, katika maandamano mjini Washington katika maadhimisho ya miaka 10 ya maandamano yaliyojulikana kama , maandamano ya watu milioni moja.
Mmoja kati ya waandaaji wa maandamano hayo , kiongozi wa taifa la Kiislamu nchini Marekani Louis Farrakhan , amesema kuwa serikali kuu imeshindwa kuwasaidia waathirika ambao wengi wao walikuwa Wamarekani weusi wakaazi wa New Orleans baada ya kimbunga Katrina.
Farrakhan , ameshauri kuwashitaki mawakala wa serikali kuu kwa kushindwa kutimiza wajibu wao wakati maafa hayo yanatokea, ambapo zaidi ya watu 1,000 wamepoteza maisha yao katika pwani ya Mexico.