WASHINGTON: Wanajeshi wa Marekani kufikishwa mahakamani
20 Oktoba 2007Matangazo
Wanajeshi 2 wa Marekani watafikishwa mbele ya mahakama ya kijeshi kwa mashtaka yanayohusika na mauaji ya raia wa Kiiraki katika mji wa Haditha nchini Irak.Inatuhumiwa kuwa Novemba mwaka 2005, wanajeshi wa Kimarekani waliwaua Wairaki 24 kulipiza kisasi kifo cha mwanajeshi mwenzao mjini Haditha.Miongoni mwa Wairaki waliouawa,10 walikuwa wanawake na watoto.