1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON

15 Februari 2005

Rais George Bush wa Marekani ameliomba Baraza la Congress la nchi hiyo liidhinishe kiasi cha dola bilioni 82 kwa ajili ya kusaidia shughuli za kijeshi nchini Iraq na Afghanistan.Kiasi hicho cha fedha kilichoombwa na Rais Bush kinafanya jumla ya fedha zilizoombewa kwa nchi hizo mbili sasa kufikia dola bilioni 300.

Ikulu ya Marekani imekiri kuwa inazidi kukwangua bajeti ya nchi hiyo ambayo sasa imepindukia na kuvunja rekodi ya dola bilioni 427.

Rais Bush amelitaka Baraza la Congress kuidhinisha haraka maombi hayo mapya ya dola bilioni 82 ambapo pia kiasi kingine cha fedha kitakwenda Pakistan,Mamlaka ya Palestina na kunyanyua msaada wa Marekani kwa waathirika wa gharika ya tsunami kufikia dola milioni 950.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW