Washington
31 Januari 2005Rais George W. Bush wa Marekani ameutaja uchaguzi wa kwanza huru kuitishwa Iraq baada ya miaka 50,kua ni ufanisi.Amesema wairaq wamedhihirisha wanataka demokrasia.Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Kofi Annan amesema wakati wa suluhu umewadia.Amewatolea mwito wairaq wa jamii ziote waashirikiane kubuni katiba mpya.Waziri mkuu wa Uengereza Tony Blair ameutaja uchaguzi huo kua ni pigo kwa magaidi.Mwenyekiti wa zamu wa umoja wa ulaya,Jean Asselborn ameshadidia wakati wa mkutano wa mawaziri wa mambo ya nchi za nje mjini Brussels,wairaq wameonyesha ujaasiri,walipopuuza onyo la magaidi na kuteremka vituoni kupiga kura.Serikali ya shirikisho mjini Berlin imeutaja uchaguzi huo wa iraq kua ni hatua muhimu kuelekea demokrasia.Katika nchi za Ghuba maoni ya wahariri yanatofautiana.Kuna wanaosifu uchaguzi huo na wengine wanaouangalia kwa jicho la tahadhari.
