1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Washington:Annan aionya tena Israel.

8 Agosti 2006

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Kofi Annan ameionya Israel kuwa mashambulizi yake katika kijiji cha Qana nchini Lebanon huenda ikawa ni sehemu ya uvunjaji wa sheria za kimataifa katika vita hivi vya Israel na Hezbollah.

Katika taarifa ya awali juu ya shambulio la July 30, Annan amewataka tena Israel na Hezbollah kuwa ni wajibu kuheshimu sheria za kimataifa.

Israel katika taarifa yake kwa Umoja wa Mataifa imesema, Qana ilikuwa ni kituo cha wanamgambo wa Hezbollah na ndipo wakatoa onyo kwa raia la kushambulia.

Lebanon katika madai yake imeyaita mashambulizi hayo kuwa ni mauaji ya halaiki, kiasi cha raia 28 waliuliwa katika shambulio la Qana wakiwemo watoto 16.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW