1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON:Bush asikitishwa na kifo cha askari mpelelezi.

8 Aprili 2005

Rais George Bush wa Marekani ametangaza kusikitishwa kwake na kifo cha askari wa upelelezi wa Italy kilichotokea kwa kupigwa risasi na wanajeshi wa Marekani alipokuwa akimsindikiza uwanja wa ndege mwandishi mmoja wa habari aliyekuwa ametekwa nyara nchini Iraq.

Rais Bush aliyasema hayo alipokutana na waziri mkuu wa Italy Silvio Berlusconi katika dhifa ya chakula cha usiku hapo jana mjini Roma.

Matokeo ya uchunguzi wa pamoja wa Marekani na Italy wa kifo cha Nicola Calipari yatatangazwa mara tu uchunguzi huo utakapo kamilika.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW