WASHINGTON:Bush ataka fedha zaidi kwa ajili ya vita vya nchini Irak
6 Februari 2007Matangazo
Rais G.Bush amewasilisha ombi la dola bilioni mia saba kwa ajili ya matumizi ya kijeshi ikiwa ni sehemu ya bajeti ya dola trilioni 2 nukta tisa anayotaka ipitishwe na bunge la nchi yake.
Sehemu kubwa ya dola hizo bilioni mia saba itatumika kwa ajili ya vita vya nchini Irak na Afghanistan.