WASHINGTON:Bush ataka vikwazo madhubuti dhidi ya Korea ya kaskazini
12 Oktoba 2006Matangazo
Rais Bush wa Marekani ameutaka Umoja wa mataifa, uiwekee vikwazo madhubuti, Korea ya Kaskazini baada ya nchi hiyo kufanya jaribio la silaha za nyuklia.
Rais Bush alitoa mwito huo alipokuwa anazungumza na wandishi habari kwenye Ikulu ya Marekani mjini Washington.
Pamoja na kusisitiza kuwa Marekani imejizatiti katika kufikia suluhisho kwa njia ya mazungumzo, rais huyo pia amesema kuwa Marekani itakuwa na haki ya kutumia njia zingine zote zilizopo.
Bwana Bush pia amesisitiza msimamo wa utawala wake kwamba hapatakuwa na mazungumzo ya ana kwa ana baina yaMarekani na Korea ya Kaskazini.