1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON:Bush aunga mkono Umoja wa Ulaya

21 Juni 2005

Rais George Bush wa Marekani amesema anaunga mkono kuwepo kwa Umoja wa Ulaya wenye nguvu.

Bwana Bush amesema hayo kwa waandishi wa habari mjini Washington baada ya kukutana na rais wa tume ya Umoja wa Ulaya bwana Jose Manuel Barroso na waziri mkuu wa Luxembourg bwana Jean –Claude Juncker .

Rais Bush pia ameeleza kwamba mahusiano baina ya Marekani na Ulaya yamo katika msingi wa maadili na malengo ya pamoja.

.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW