WASHINGTON:Fischer yuko Washington
17 Novemba 2003Matangazo
Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Yoschka Fischer amewasili mjini Washington ambapo mazungumzo yake na maafisa wa serikali ya Marekani yanatarajiwa kulenga suala la Iraq. Fischer anatazamiwa leo hii kukutana na waziri wa mambo ya nje wa Marekani Colin Powell na mshauri wa usalama wa taifa Condeleeza Rice. Baadae wiki hii Fischer ataelekea New York kwa mazungumzo katika Umoja wa Mataifa.
