WASHINGTON:Maendeleo katika mazungmzo ya Korea Kaskazini
9 Agosti 2005Matangazo
Kwa mujibu wa Marekani,mazungumzo ya pande 6 kuitaka Korea ya Kaskazini iachilie mbali mradi wake wa kutengeneza silaha za kinuklia,yamefanya “maendeleo muhimu”.Msemaji katika Ikulu ya Marekani amesema,kuna muafaka wa mawazo kuwa silaha za kinuklia zisiwepo kwenye rasi ya Korea.Lakini baada ya kukutana kwa siku 13 kwa mfululizo bila ya kupata makubaliano, wanadiplomasia siku ya jumapili waliamua kupumzika mpaka tarehe 29 Agosti.Kwa mujibu wa maafisa,majadiliano yamekwama kuhusika na dai la Korea ya Kaskazini la kutaka kiwanda cha nishati ya kinuklia.