WASHINGTON:Marekani kutoa muda zaidi kwa Korea Kaskazini juu ya suala la Nuklia
2 Mei 2007Matangazo
Marekani imeonyesha nia ya kutaka kuipa Korea Kaskazini muda zaidi wa kuchukua hatua ya kutekeleza ahadi yake ya mwezi Februari ya kukomesha mpango wake wa Kinuklia.
Hata hivyo Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Condoleeza Rice amesema subira ya ulimwengu haitakoma.
Ametoa matamshi hayo baada ya kukutana na mawaziri wa mambo ya nje wa na ulunzi wa Japan.
Bibi Rice amesmea anatambua kwamba serikali ya mjini Pyongyanga hivi karibuni imekuwa ikionyesha kujitolea katika kutekeleza ahadi iliyoitoa mwezi wa Februari ya kuachana na mpango wake wa Kinuklia.
Korea Kaskazini imesita kutekeleza ahadi hiyo hadi pale mzozo unaohusu fedha zake dolla milioni 25 zilizozuiliwa kwenye benki ya Macau China utakapotatuliwa.