WASHINGTON.Mazungumzo ya WTO
31 Julai 2006Rais George W Bush wa Marekani na waziri mkuu wa Uingereza Tony Blair wamekubaliana kujaribu tena kuya anzisha mazungumzo yaliyokwama ya shirika la biashara ulimwenguni WTO.
Waziri mkuu wa Uingereza amesema kwamba huenda mazungumzo hayo yakaanza tena katika muda wa wiki chache zijazo.
Viongozi hao waliafikia uamuzi huo baada ya kukutana katika ikulu ya White House mjini Washington.
Mazungumzo ya shirika la biashara ulimwenguni yalikwama tarehe 24 julai baada ya jitahada za miaka mitano za kutaka kuyafanikisha mazungumzo hayo.
Mkuu wa shirika la bishara ulimwenguni bwana Pascal Lamy mwishoni mwa wiki alisimamisha mazungumzo ya kibiashara ya duru ya Doha kufuatia kushindwa kwa dola sita kubwa kukubaliana juu ya kuondoa vikwazo vya ushuru na juu ya swala la ruzuku kwa wakulima.