WASHINGTON:Rais Bush hatojifungamanisha na azimio la Irak
16 Februari 2007Matangazo
Rais George W.Bush wa Marekani amesema hatojifungamanisha na azimio litakalopitishwa na bunge kuhusu Irak,isipokuwa mswada wa azimio unaohusika na ombi la kuongeza pesa kwa ajili ya vikosi vya Marekani nchini Irak.Leo Baraza la Wawakilishi la Marekani linapiga kura na kesho Jumamosi,Seneti pia itapiga kura kuhusu azimio hilo ikiwa Marekani ipeleke wanajeshi 21,500 wengine nchini Irak.