1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Washington:Waziri wa Vietnam ziarani Marekani:

11 Novemba 2003
Waziri wa Ulinzi wa Vietnam, kwa mara ya kwanza kabisa baada ya kumalizika vita vya Vietnam mwaka 1975, anaitembelea rasmi Marekani. Phan Van Tra amezungumza mjini Washington na Waziri mwenzake Donald Rumsfeld. Taarifa iliyotolewa na Wizara ya Ulinzi ya Marekani, Pentagon, imesema kuwa Mabwana Tra na Rumsfeld wamezungumzia uwezekano wa kuboresha ushirikiano wao katika nyanja za ulinzi. Mazungumzo yao yameimarisha tena uhusiano wa masuala ya kiulinzi kati ya Vietnam na Marekani. Vietnam imeiomba pia msaada Marekani wa kupambana na athari za kemikali za sumu zinazoathiri afya zilizotumiwa na Wamarekani wakati wa vita. Wavietnam kadhaa ni wagonjwa kutokana na kemikali hizo zinazojulikana kama "Agent Orange." Nchi hizi mbili zimerudishiana uhusiano wa kibalozi mwaka 1995 na baadaye kutia saini mkataba wa kushirikiana kibiashara.
Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW