1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroMarekani

Marekani kutuma silaha Ujerumani kukabili kitisho cha Urusi

11 Julai 2024

Marekani itaanza kupeleka makombora ya masafa marefu nchini Ujerumani kuanzia mwaka 2026, hatua muhimu inayolenga kudhibiti ongezeko la kitisho cha Urusi barani Ulaya..

Marekani | Mkutano wa Nato | Washington | Biden, Scholz na Stoltenberg
Rais Joe Biden ambaye ni mwenyeji wa mkutano wa kilele wa NATO akipeana mkono na Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz, ambae wameingia makubaliano ya silaha. Kulia ni katibu mkuu wa NATO, Jens StoltenbergPicha: Evan Vucci/AP Photo/picture alliance

Chini ya makubaliano ya mataifa hayo yaliyotangazwa kwenye mkutano wa kilele wa NATO mjini Washington, Marekani itapeleka silaha nzito kabisa ambazo haijawahi kuzipeleka Ulaya tangu enzi ya Vita Baridi, likiwa ni onyo la wazi kwa Rais Vladimir Putin.

Taarifa yao ya pamoja ilisema maandalizi ya kupelekwa silaha hizo kwa awamu, ambazo ni pamoja na makombora ya masafa marefu, yanafanyika.

Hatua hiyo pengine ingezuiwa chini ya makubaliano ya Nyuklia kati ya Marekani na uliokuwa Umoja wa Sovieti ya mwaka 1987, yaliyovunjika mwaka 2019.

Kwenye mkutano huo, wakuu wa ushirika wa NATO aidha walikubaliana kuiongezea Ukraine msaada wa kijeshi wa karibu dola bilioni 40 mwaka ujao.