Washirika wakusanyika Paris kujadili mustakabali wa Ukraine
6 Januari 2026
Wajumbe hao wanaendeleza juhudi za kuikamilisha mipango ya inayosimamiwa na Marekani ya kumaliza vita vya Urusi nchini Ukraine. Mkutano wa kilele wa kundi la washirika wa Ukraine liliopewa jina la "Muungano wa Wenye Nia ya kuisaidia Ukraine" ni wa hivi karibuni kati ya mikutano kadhaa iliyopangwa kwa mwaka mpya huku juhudi za kidiplomasia za kukomesha mzozo huo ambao ndio mbaya zaidi barani Ulaya tangu Vita vya Pili vya Dunia, zikishika kasi katika wiki za hivi karibuni.
Wawakilishi wa nchi 35, wakiwemo wakuu wa nchi 27, watakusanyika mjini Paris, huku Ufaransa ikisema mkutano huo unalenga kuonyesha "mwelekeo" kati ya Washington, Kyiv na washirika wa Ulaya kuhusu dhamana za usalama kwa Ukraine.
Mjumbe maalum wa Rais Donald Trump wa Marekani Steve Witkoff na mkwewe Jared Kushner watahudhuria mkutano wa muungano huo.