1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUrusi

Miito yaanza kutolewa Urusi ya kurejeshwa adhabu ya kifo

24 Machi 2024

Maafisa wa ngazi za juu katika serikali ya Rais Vladimir Putin wametoa wito kwa taifa hilo kurejesha adhabu ya kifo baada ya shambulizi la siku ya Ijumaa kwenye tamasha mjini Moscow.

Urusi | Dmitri Medvedev
Naibu Mwenyekiti wa Baraza la Usalama la Urusi Dmitry Medvedev amemtolea wito Rais Vladimir Putin kurejesha adhabu ya kifo kwa wauaji na magaidiPicha: Alexei Maishev/TASS/IMAGO

Urusi ilisitisha adhabu ya kifo tangu miaka ya 1990.

Naibu mkuu wa kamati ya usalama ya Bunge la Urusi-Duma Yury Afonin amesema jana kwamba ni muhimu kurejesha adhabu hiyo linapokuja suala la ugaidi ama mauaji.

Washirika wa karibu wa Putin, Rais wa zamani, ambaye sasa ni naibu mwenyekiti wa Baraza la Usalama la Urusi Dmitry Medvedev pamoja na Spika wa bunge la nchi hiyo Vyacheslav Volodin nao wametaka magaidi "kumalizwa" kufuatia shambulizi hilo.

Hata hivyo, wakosoaji wameonyesha wasiwasi juu ya mipango hiyo, na hasa kutokana na Urusi kuzitumia sheria zake za kupambana na ugaidi na itikadi kali kuwalenga wapinzani na wanaoiunga mkono Ukraine.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW