1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Migogoro

Washirika Ulaya wataka kuimarisha sekta ya silaha ya Ukraine

14 Januari 2025

Mawaziri wa ulinzi kutoka mataifa matano ya Ulaya wamekubaliana kuimarisha sekta ya silaha ya Ukraine na kujadili usalama wa Ulaya katika muundo mpya wa ushirikiano kufuatia tishio la Donald Trump kuhusu ulinzi wa NATO.

Ubelgiji Mawaziri wa nje wa EU Brussels | Kaja Kallas
Mkuu wa sera ya kigeni wa Umoja wa Ulaya Kaja KallasPicha: Virginia Mayo/AP Photo/picture alliance

Mawaziri wa ulinzi kutoka Poland, Ujerumani, Ufaransa, Italia na Uingereza waliokutana mjini Warsaw jana Jumatatu wamekubaliana kuimarisha juhudi za kuijengea uwezo sekta ya silaha ya Ukraine hasa wakati huu inapopambana na Urusi.

Waziri wa ulinzi wa Ujerumani Boris Pistorius amesema iwapo Ukraine itakuwa na uwezo wa kutengeneza silaha nchini humo, basi itakuwa rahisi zaidi kulihami jeshi lake kwa vifaa na silaha.

Soma pia: Mgogoro wa Ukraine na Urusi: Mashambulizi ya droni, diplomasia ya kimataifa, na mustakabali wa amani

Mawaziri hao pia wamejadili masuala ya usalama wa Ulaya katika muundo mpya wa ushirikiano wa mataifa matano uliobuniwa kufuatia ushindi wa Donald Trump katika uchaguzi wa urais.

Rais huyo mteule wa Marekani ametishia kutozilinda nchi za jumuiya ya NATO ambazo zitakosa kuongeza bajeti zao za ulinzi hadi asilimia tano ya pato jumla la taifa.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW