1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMarekani

Washukiwa wa 9/11 wafikia mpango kupunguziwa adhabu

1 Agosti 2024

Wizara ya Ulinzi ya Marekani imesema jana kwamba washitakiwa watatu waliohusishwa na mashambulizi ya Septemba 11, 2001 wameingia makubaliano ya kukiri mashtaka ili kupunguziwa adhabu.

Kesi ya mashambulizi ya Septemba 11
Washitakiwa watatu Septemba 11, 2001 wameingia makubaliano ya kukiri mashtaka ili kupunguziwa adhabuPicha: Janet Hamlin/AP Photo/picture alliance

Pentagon hata hivyo imesema masharti hasa ya makubaliano hayo hayatatolewa hadharani kwa sasa, ingawa gazeti la New York Times liliripoti, walikiri ili badala yake wahukumiwe kifungo cha maisha badala ya kifo.

Soma pia: Kengele yasikika wakati Marekani ikiadhimisha kumbukumbu za mashambuliyi za Septemba 11

Khalid Sheikh Mohammed, anayedaiwa kuandaa mashambulizi hayo, alikuwa miongoni mwa washitakiwa hao wanaozuiwa kwenye gereza la Guantanamo Bay.

Soma pia: FBI waweka hadharani uchunguzi wa Septemba 11 kwa amri ya Rais Biden

Wanakabiliwa na makosa ya kuja njama, ugaidi na mauaji ya watu 2,976 kufuatia mashambulizi kwenye kituo cha Kimataifa cha Biashara mjini Washington, Pentagon kwenyewe na uwanja wa Shanksville, Pennysylvania.