Wasichana wa Chibok waungana na wenzao
31 Mei 2017Matangazo
Aisha Alhassan, waziri wa masuala ya wanawake na maendeleo ya kijamii, amesema jana kwamba wanawake hao watahudhuria miezi kadhaa ya mafunzo kwa ajili ya kuwabadilisha.
Ndani ya kipindi hicho, watakuwa na madaktari na wauguzi kuwasaidia kupona kutoka katika fadhaa ya miaka mitatu wakiwa katika maisha ya kutekwa nyara.
Hata hivyo, kumekuwa na ukosowaji mkali juu ya namna wasichana hao walioachiwa huru walivyobakia katika mji mkuu wa Nigeria, Abuja, badala ya kujiunga na familia zao. Alhassan amesema wasichana hao wako mjini Auja kwa idhini yao wenyewe.