Wasiwasi kuhusu Kombe la Dunia Qatar 2022
20 Septemba 2013Taifa hilo lenye utajiri wa nishati, ambako nyuzijoto hufikia sentigredi 45 ilipewa kibali cha kuandaa Kombe la Dunia miaka mitatu iliyopita katika uamuzi wa kushangaza.
Qatar inasema inaweza kukubali kuhamisha dimba hilo hadi msimu wa baridi lakini ikasisitiza kuwa licha ya joto kali, inaweza kuandaa Dimba la Dunia msimu wa joto kwa kujenga viwanja vyenye hewa ya baridi kwa kutumia teknolojia mpya inayojali mazingira.
Namna ambavyo mashabiki wataweza kukabiliana na joto, nje ya viwanja, bado ni suala linalotia wasiwasi na Rais wa FIFA Sepp Blatter hivi karibuni amesema lilikuwa kosa kupanga kinyang'anyiro hicho cha msimu wa joto, katika taifa la jangwa.
Rais wa Shirikisho la Soka barani Ulaya UEFA, Michel Platini pia amethibitisha kuwa mashirkisho 54 wanachama wa UEFA wamekubaliana kwa kauli moja kuhusu wazo la kuhamisha dimba hilo la Qatar, hadi msimu mwingine wa mwaka
Lakini nayo kamati andalizi ya Qatar imejaribu kuondoa wasiwasi hiyo, kwa kusema teknolojia ya kuleta hewa ya baridi, kwa kutumia solar, katika maeneo ya umma, nje na ndani ya viwanja, huenda ikatatua shida hizo. bila shaka tutasubiri kuona jinsi namna suala hilo litakavyokwenda, nasi tutakufahamisha
Mwandishi: Bruce Amani/AFP
Mhariri:Yusuf Saumu