1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wasiwasi wa Tsunami Barani Ulaya

Saumu30 Desemba 2004

Gharika yaTsunami imeongeza wasiwasi kwa jamii ya mataifa ya Ulaya baada ya kutoweka kwa takriban watalii 5000.Watalii hao nusu yao wakiwa raia wa Sweden na Ujerumani wametoweka kwa siku ya nne hii leo, baada ya Zilzala hiyo kuvunjilia mbali mahoteli yaliokuwa ufukoni mwa bahari, barani Asia.

Gharika kuu ya Tsunami iliyowaua maelfu ya watu barani Asia
Gharika kuu ya Tsunami iliyowaua maelfu ya watu barani AsiaPicha: AP

Kimbunga hicho cha bahari kilichoingia kwa kishindo kikubwa barani Asia mwishoni mwa wiki iliyopita, kimeyagharimu maisha ya maelfu ya watu na kuwaacha mamilioni ya wengine bila makao.Idadi ya walioangamizwa na mawimbi hayo mazito ya Tsunami,inazidi kuongezeka kila kukicha na kuzua wasiwasi zaidi barani ulaya.kufikia wakati huu zaidi ya watu 82 elfu wamekwisha uwawa katika balaa hilo lilovamia nchi ya Srilanka,Indonesia,India,Thailand,Malaysia,na nchi kadha barani Afrika.

Ingawa idadi rasmi ya watalii waliokufa imetangazwa kuwa 212 na nchi zao, serikali ya Thailand imetangaza kuwa watalii takriban ya 435 wamekufa nchini humo. Idadi ya watalii walioripotiwa kutoweka kufikia sasa, ni pamoja na watalii 1500 kutoka sweden,wajerumani 1000,wataliano 600,watalii 464 wa Norway,219 wa Danemark,200 kutoka finnland na 200 kutoka Czech pamoja na watalii 294 kutoka nchi ya Singapore.

Kansela wa Ujerumani Gerhard Schroeder amewaambia wananchi wake katika mkutano na wandishi habari kwamba matarajio yaliyopo kuhusu raia wake walioripotiwa kutoweka, ni kuwa wamekufa, hasa ikizingatiwa Ukubwa wa dhoruba iliyosababishwa na Zilazala hiyo.

Huku sikukuu ya mwaka mpya ikiingia kwa maombolezi waokoaji wanaotafuta maiti pamoja na manusura wamesema, wanatarajia kupata watalii zaidi waliokufa katika kisiwa kilichoko upande wa kaskazini mwa ufuko wa bahari ya Khao lak ,ambako ndio maficho zaidi ya watalii kutoka Scandinavia na Ujerumani wanaokimbia baridi kali nchini mwao.

Maombolezi yanatarajiwa kuigubika sikukuu ya mwaka mpya kote barani ulaya.Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Joshka Fischer amewaataka wananchi wa ujerumani kutoa pesa zao katika kuwasaidia waathiriwa wa balaa la Tsunami badala ya kununua fataki za kuukaribisha mwaka mpya.Nchini Sweden bendera zitapeperusha nusu mlingoti.Hata hivyo vyombo vya habari nchini Sweden vimeishutumu serikali yake kwa kupuuza balaa hilo huku asilimia 64 ya raia wake wakihisi serikali haijafanya mengi kusaidia waathiriwa wa Tsunami.

Kansela wa Ujerumani Gerhad Schroder, amezitaka nchi tajiri kuangalia uwezekano wa kuzisamehe madeni nchi zilizokubwa na maafa ya Tsunami ikiwa ni pamoja na Somalia na Indonesia.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW