Wasiwasi waongezeka kuhusu mzozo wa Iran
27 Februari 2026
Juhudi za kuepusha vita kati ya Iran na Marekani zinaendelea, ambapo waziri wa mambo ya nje wa Oman atakutana leo Ijumaa na makamu wa rais wa Marekani JD Vance mjini Washington. Hata hivyo kwa upande mwingine,Marekani imeruhusu kuondoka kwa raia wake wasiokuwa na kazi za dharura kutoka nchini Israel.
Chanzo kinachofahamu kuhusu mvutano huu,kimeliambia shirika la habari la Reuters kwamba waziri wa mambo ya nje wa Oman, Sayyid Badr Albusaid atakuna na makamu wa rais wa Marekani mjini Washington,baada ya kufanyika mazungumzo ya kujaribu kuepusha uwezekano wa Marekani kuishambulia Iran, katika wakati ambapo Washington imeshakusanya nguvu zake za kijeshi.Marekani na Iran zakubaliana kuendelea kuzugumza
Jana mazungumzo kati ya Iran na Marekani chini ya usimamizi wa Oman huko Geneva ambayo yalitajwa kama ni juhudi za mwisho za kidiplomasia kwenye mzozo huu yalipoteza matumaini baada ya Tehran kuionya Washington, kwamba inapaswa kuacha kutowa mapendekezo mengi kupita kiasi kama masharti ya kufikia makubaliano.
Na wakati ulimwengu ukisubiri kuona kitakachojitokeza kwenye mazungumzo ya leo huko Washington, Hali ya wasiwasi kuhusu kutokea vita imeichochea China hivi leo kujiunga na mataifa mengine kuwatahadharisha raia wake kuondoka nchini Iran haraka iwezekanavyo.
Lakini hata Marekani yenyewe, imeidhinisha hatua ya kuondoka kwa wafanyakazi wa ubalozi wake nchini Israel wasiokuwa na majukumu ya dharura,huku manuari yake kubwa ya kijeshi USS Gerald R Ford ikiwa inatarajiwa kuwasili kwenye pwani ya Israel ambayo ni mshirika mkubwa wa Marekani.
Ubalozi wa Marekani nchini Israel umeandika ujumbe kwenye tovuti yake ukiwahimiza raia wake wanaotaka kuondoka Israel watumie fursa ya kuwepo bado kwa ndege zinazosafiri kutoka nchini humo.Mzozo wa Israel na Iran
Gazeti la Newyork Times limeripoti kwamba balozi wa Marekani, Israel, Mike Huckabee pia amewatumia barua pepe wafanyakazi wa ubalozi huo akiwaambia wanaotaka kuondoka wanapaswa kufanya hivyo leo Ijumaa. Itakumbukwa kwamba Februari 19 rais Donald Trump aliipatia muda wa siku 15 Jamhuri ya kiislamu ya Iran kufikia makubaliana.
Mvutano mkubwa unaoleta kizingiti cha kufikiwa makubaliano ni kwamba Iran inasisitiza mazungumzo yajikite kwenye masuala yanayohusu mpango wake wa Nyuklia tu,na sio mambo mengine Marekani inataka kujadili pia mradi wa makombora wa Tehran pamoja na suala la Iran kuunga mkono makundi ya wanamgambo ambayo ni waitifaki wake.
Iliripotiwa jana na gazeti la Wall Street la Marekani kwamba timu ya mazungumzo ya rais Trump itaitaka Iran kuaharibu kabisa vituo vyake vitatu vya shughuli za Nyuklia na kukabidhi madini yake yote ya Urani yaliyorutubishwa kwa Marekani.
Lakini hivi leo waziri wa mambo ya nje wa Iran Abbas Aragchi bila kuyataja mapendekezo ya Washington, alisema ili yawepo mafanikio kwenye njia ya mazungumzo haya kunahitajika umakini na kuzingatiwa uhalisia kutoka upande wa pili na kujiepusha kufanya makosa pamoja na kuweka mapendekezo ya kupita kiasi.Hezbollah
Pamoja na yote hayo ripoti zinasema, shirika la kimataifa la kudhibiti nguvu za Nyuklia IAEA nalo limesema majadiliano kuhusu mpango wa Nyuklia wa Iran yatafanyika wiki ijayo.