1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wasiwasi watawala kuhusu mustakabali wa serikali ya Merz

22 Desemba 2025

Uchunguzi mpya uliofanywa nchini Ujerumani umeonyesha karibu nusu ya Wajerumani wana wasiwasi ikiwa muungano wa serikali unaoongozwa na wahafidhina utadumu hadi uchaguzi ujao.

Ujerumani Berlin 2025 | Kansela Friedrich Merz wakati wa kipindi cha maswali kwa serikali katika Bunge la Ujerumani
Kansela Friedrich Merz (CDU) akijibu maswali kutoka kwa wabunge wakati wa kikao cha 49 cha Bunge la Ujerumani mjini Berlin, Desemba 17, 2025Picha: Jens Krick/Flashpic/picture alliance

Kura ya maoni iliyofanywa na taasisi ya YouGov kwa ajili ya shirika la habari la DPA imeonyesha asilimia 49 hawatarajii serikali kumaliza muhula wake, huku asilimia 17 wakitabiri kusambaratika kwa muungano huo mapema mwakani.

Baada ya miezi saba na nusu iliyogubikwa na migogoro, ni asilimia 9 tu ya waliohojiwa wanaamini hali itarejea kawaida mwakani, huku asilimia 49 wakitarajia mvutano kuendelea na asilimia 21 wakiamini hali kuwa mbaya zaidi.

CDU/CSU ilishinda kwa asilimia 28.5 na SPD kwa asilimia 16.4 za kura, lakini pande zote mbili zimeanguka vibaya na kukosa wingi wa kura katika tafiti za karibuni, vyama vya CDU/CSU vikiwa na asilimia kati ya 24 na 27 na SPD kikiwa na asilimia kati ya 13 na 14.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW