1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wasomali wapewa hifadhi nchini Kenya.

26 Novemba 2007

Nairobi.

Serikali ya Kenya imewakabidhi Wasomali 22, kwa shirika la umoja wa mataifa la kuwahudumia wakimbizi. Wengi wa Wasomalia hao wakiwa wanawake na watoto, wamekuwa kwa muda wa wiki mbili wakiishi katika chumba cha kungojea ndege katika uwanja wa ndege wa mjini Nairobi. Maafisa wa idara ya uhamiaji nchini Kenya wamewasafirisha watu hao ambao walikuwa wakiomba hifadhi ya kisiasa kutoka katika uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta kwenda katika kambi ya wakimbi ya Daadab kaskazini mashariki ya Kenya siku ya Jumamosi.

Wasomali hao ni miongoni mwa wakimbizi 100 ambao wamepelekwa mjini Entebe nchini Uganda kupitia katika mji mkuu Nairobi , Novemba 12. Maafisa wa Uganda waliwarejesha siku hiyo hiyo nchini Kenya, wakisema kuwa wametumia hati za kusafiria ambazo zimefutwa na serikali ya mpito ya Somalia iliyowekwa madarakani mwaka 2004.