Wasoshalisti kubadili siasa ya mambo ya nje ya Uspania.
16 Machi 2004MADRID/WASHINGTON: Baada ya ushindi wao wa kushangaza katika uchaguzi wa bunge, Wasoshalisti wa Uspania wananuiya kubadili siasa ya yao ya mambo ya nje. Akiwa ni Mkuu wa Chama cha Wafanaya Kazi, Waziri Mkuu mteule José Luis Rodrígues Zapatero amesema ana niya ya kuwiyanisha siasa yake na ile washirika wa Ulaya, Ujerumani na Ufaransa waliyoochukua msimamo wa kupinga vita vya Iraq. Wale wanajeshi 1300 wa Uspania waliyoko Iraq watarejeshwa nyumbani kabla ya Juni 30 ikiwa hawatopata kibali rasmi cha Umoja wa Mataifa cha kubakia huko, alisisitiza. Hadi sasa Marekani haikujibu moja kwa moja shabaha hizo za Uspania. Yanaweza yakazingatiwa mabadiliko katika harakati za wanajeshi wa kimataifa nchini Iraq, ilisema taarifa kutoka Washington. Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani Adam Ereli alisema katika swali la kuwekwa madarakani serikali mpya ya mpito mjini Baghdad huenda litahitajika azimio jipya la UM kuhusu Iraq.