1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMisri

Wasuluhishi wasukuma majadiliano ya kusitisha vita Gaza

6 Machi 2024

Wasuluhishi wa kimataifa na wawakilishi wa kundi la Hamas wako mjini Cairo kwa mazungumzo ya kujaribu kufikia makubaliano ya kusitisha vita vya Ukanda wa Gaza kuelekea kuanza kwa mwezi mtukufu wa Ramadhan.

Hali ya Ukanda wa Gaza
Hali ya Ukanda wa Gaza Picha: Mohammed Salem/REUTERS

Wajumbe wa kundi la Hamas linalotawala Ukanda wa Gaza pamoja na wale wa Marekani wanatarajiwa kukutana na wasuluhishi wa Misri na Qatar kwa siku ya tatu ya mazungumzo kuhusu mkataba wa usitishaji mapigano kwa muda wa wiki sita.

Mkataba huo unajumuisha masharti ya kuachiwa raia wa Israel wanaoshikiliwa mateka kwa mabadilishano na wafungwa wa Kipalestina wanaozuiliwa kwenye magereza nchini Israel.

Kadhalika utahusisha upelekeaji msaada zaidi wa kiutu ndani ya Ukanda wa Gaza ambako inaarifiwa hali ya kibinadamu inazidi kuwa mbaya.

Hata hivyo Israel haishiriki mazungumzo hayo ya mjini Cairo licha ya shinikizo la kidiplomasia la kutaka yapatikane makubaliano ya kusitisha vita kabla ya kuanza mfungo wa mwezi wa Ramadhan mnamo wiki ijayo.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW